Ijumaa, Januari 15, 2016

KUFANIKIWA KATIKA UMRI MDOGOSI KITU CHA AJABU, JITAHIDI KUZINGATIA HAYA

1. Zifuate nafasi za kufanikiwa zilipo, usikae ukisubiri zikufuate. Kama kilimo cha vitunguu ni Mbeya, wewe Dar hapakufai, nenda uone mambo yanaendaje. Kama dili za mawe ziko Geita na Arusha fuata zilipo. Kama elimu iko kwenye vyuo wewe mtaani panakuzingua tu. Elimu haitakufuata wala mali haikufuati. Mafanikio unayatafuta, hayakutafuti ndugu yangu.

2. Kuwa na mshauri mzuri. Mjomba, rafiki yake baba, boss wako, mfanyakazi mwenzako mwenye experience zaidi ya maisha, etc. Hawa watu huwa wameona mbali kabla yako na kama wako wazi katika mioyo yao basi watakupa walau mwanga wa jinsi ya kujipanga na mambo. Ukichukua mawazo yao ukachanganya na yako na mkono wa Mungu mambo safi.

3. Usiweke mayai yako yote katika kapu moja. Pambana huku na kule. Sawa unalipwa labda mshahara wa laki 6 kwa mwezi. Hata siku moja hizo akiba za laki laki hutaweza kuhama ulikopanga na kujenga kwako. Lakini hizo laki laki ukiziwekeza mahali baada ya miaka mitatu huku kazi inaendelea utakuwa tofauti. I am telling you!

4. Ziba masikio. Ukisikiliza sana ya watu hutafanya lolote kwenye maisha. Mara fulani yuko hivi mara yuko vile. Sio ishu. Wewe muamini Mungu wako na fanya yako. Watu wataongea tu haijalishi unafanya mazuri au mabaya so focus on your things na Mungu wako na mipango yako.

0 comments:

Chapisha Maoni