Jumatano, Januari 13, 2016

KITUO CHA CHANJO CHAPIGWA BOMU, 15 WAFA NA 20 KUJERUHIWA

Watu 15 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu lililolenga maafisa wa usalama nje ya kituo cha utoaji chanjo ya ugonjwa wa kupooza (polio) mjini Quetta huko kusini magharibi mwa Pakistan.
Duru za tiba zimesema kuwa, maafisa wa polisi 12 na raia 2 ni miongoni mwa watu 15 waliouawa katika mripuko huo mapema leo. Walioshuhudia wanasema kuwa, baada ya mripuko mkubwa wenye kishindo kusikika, ilifuata milio ya risasi kwa dakika kadhaa katika eneo hilo. Pakistan imezindua kampeni ya siku 3 ya kutoa chanjo ya ugonjwa wa polio katika wilaya za mkoa wa Balochistan, ikilenga watoto milioni 2.4 walio chini ya miaka 5. Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni