Jumatano, Januari 13, 2016

BOTI 2 ZA KIJESHI ZA MAREKANI ZINASHIKILIWA IRAN

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limethibitisha kuwa Iran inazuilia boti 2 za jeshi la majini la Marekani kwa kuingia katika maji ya nchi hii kinyume cha sheria.
Taarifa ya IRGC iliyotolewa mapema leo Jumatano imesema kuwa, boti hizo za kijeshi za US zimenaswa ndani ya maji ya Iran katika Ghuba ya Uajemi zikiwa na mabaharia 10. Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa boti hizo zilikuwa katika manuva ya kijeshi kati ya maji ya Kuwait na Bahrain na moja yao ikapoteza mwelekeo baada ya kukumbwa na hitilafu za kiufundi na kuingia katika maji ya Iran. Imearifiwa kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani John Kerry amewasiliana kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif kuhusiana na kadhia hiyo. Peter Cook, Msemaji wa Pentagon amenukuliwa na shirika la habari la Associated Press akisema kuwa, Tehran na Washington zinafanya mawasiliano kuhusu suala hilo huku akitaraji kuwa mabaharia hao wa Marekani wataachiwa huru karibuni hivi.

0 comments:

Chapisha Maoni