Jumatano, Januari 13, 2016

KOREA KASKAZINI KUWEKEWA VIKWAZO BAADA YA JARIBIO LA BOMU WIKI ILIYOPITA

Bunge la wawakilishi nchini Marekani limepitisha sheria itakayowezesha Marekani kuweka vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini (DPRK) baada ya taifa hilo kufanya majaribio ya bomu aina ya nyuklia.
Uamuzi huo ambao ulipitishwa kwa kura 418 dhidi ya 2 inampa rais wa Marekani uwezo wa kuamuru vikwazo dhidi ya wanaoshiriki na Korea kaskazini katika biashara aina ya silaha hatari, bidhaa za kifahari, wizi wa pesa, kutengeneza bidhaa ghushi ikiwemo shughuli zingine zinazokiuka haki za binadamu.

0 comments:

Chapisha Maoni