Jumamosi, Januari 23, 2016

KIMBUNGA CHA BARAFU CHAIPIGA MAREKANI

Kimbunga kikali cha theluji kinachobashiriwa kuwa kikubwa zaidi kwa muda wa miaka mia moja kimewasili katika ufukwe wa Mashariki mwa Marekani.
Eneo linalotarajiwa kukabiliwa vikali ni mji mkuu wa Washington DC, ambako hali ya hatari tayari imetangazwa.
Afisi za wafanya kazi wa Serikali na shule zilifungwa mapema na huduma za usafirishaji pia kusitishwa.
Mwandishi wa BBC alisema kuwa mji huo ni kama uliohamwa kwa kuwa watu wote wamejifungia manyumbani hadi kimbunga hicho kitakapopita.
Mji wa New York pia umetangaza hali ya hatari ya hali ya hewa.
Kumekuwa na visa zaidi ya 1,000 vya magari kugongana katika Caroline Kaskazini pekee.
Zaidi ya watu milioni 50 wameonywa kuwa watarajie barafu ya kina cha zaidi ya futi mbili, itakayoongezeka kutokana na kimbunga na upepo mkali utakaovuma saa chache zijazo.

0 comments:

Chapisha Maoni