Jumapili, Januari 24, 2016

CELINE DION AMUAGA KAKA YAKE, NI SIKU MBILI BAADA YA MAZISHI YA MUMEWE RENE ANGELIL

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Canada, Celine Dion jana alihudhuria ibada ya kumuaga kaka yake Daniel Dion ikiwa ni siku moja baada ya kumzika mumewe René Angélil.
Katika ibada hiyo, Celine aliambatana na mama yake pamoja na dada yake huko Quebec, Canada kumuaga kaka yake huyo aliyefariki wiki moja iliyopita baada ya kuugua saratani ya koo, ubongo na ulimi.
Maziko ya Daniel yatafanyika kesho (Jumatatu) huko Charlemagne, Quebec nchini Canada ambapo familia yake ilikulia.
Tofauti na mazishi ya mume wa Celine yaliyofanyika juzi (Ijumaa) huko Notre-Dame Basilica, Canada ibada ya kumuaga kaka yake ilihudhuriwa na watu wachache wengi wao wakiwa wanafamilia. Watoto watatu wa Celine; René Charles na mapacha Nelson na Eddy nao hawakuhudhuria ibada hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni