CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mbeya Mjini
kimetoa siku tatu kwa Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi,
kukanusha kauli yake aliyotoa hivi karibuni ya kuwa atawafanyia “kitu
mbaya”wafuasi wa chama wakiendelea na msimamo kuandamana.
Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini walisema kuwa
wanasikitishwa kamanda huyo kutoa kauli hiyo yenye lengo la kuwatishia
usalama raia aliokabodhiwa jukumu la kuwalinda na mali zao.
Hivi karibuni Kamanda Msangi, alikaririwa na vyombo mabalimbali vya
habari kwa nyakati tofauti kuwa kama CHADEMA wataendelea na msimamo wa
kuandamana polisi watawafanyia kitu kibaya.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya
ya Mbeya Mjini John Mwambija, alisema wamepata taarifa baadhi ya
viongozi wakuu wanne wa chama hicho wamelengwa kuuawa.
Mwambija alisema awali walitoa siku tano kwa kiongozi huyo ili
akunushe kauli hiyo waliyodhani ametekeleza lakini kwakuwa hajaomba
radhi wanaamini alidhamiria.
Naye mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’alisema
anasikitishwa na kauli ya kamanda Msangi inayohatarisha amani, umoja na
mshikamano kwenye jamii.
Nadhani kinachomponza kamanda Msangi ni ugeni au cheo alichopewa….. anashindwa kukitumia kama wenzake walivyofanya wakati wakiwa hapa
alisema
0 comments:
Chapisha Maoni