Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya
kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti
chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la kitaifa la
mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa
Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa
kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi
Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa
kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho
kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa
katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia
baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho
kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha
kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji
alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani
yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake
vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo
alisema jaji.
Jaji
alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama
ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi
ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey
kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya
kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake
za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.




0 comments:
Chapisha Maoni