Jumatano, Oktoba 08, 2014

MUETHIOPIA AKAMATWA MBEYA, KISA HIKI HAPA

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia raia na mkazi wa nchini Ethiopia aitwaye Seyim Latabo (45) kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Mhamiaji huyo alikamatwa jana majira ya saa 07:50 asubuhi huko katika stendi ya mabasi – Tukuyu, kata ya Kawetele, tarafa ya Tukuyu mjini, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ameshafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wageni kufuata taratibu za kuingia nchini ili kuepuka matatizo na madhara yanayoweza tokea.

0 comments:

Chapisha Maoni