Ijumaa, Oktoba 03, 2014

KANISA KATOLIKI TZ: MCHAKATO WA KATIBA NI MATAKWA YA CCM

MAKAMU wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amesema licha ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kupitishwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba jana, kelele za kudai Katiba Mpya hazitaisha kwani mchakato wa upatikanaji wake haukuwa wa maridhiano.
Askofu Niwemugizi alisema mchakato mzima umeendeshwa kwa mtazamo, matakwa na mapenzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kwa maana hiyo, kelele za Katiba Mpya zitaendelea na kutahadharisha kuwa hali hiyo ni hatari kwa usalama wa nchi.
Sichukii chama chochote na wala mimi si mwanachama wa chama chochote, lakini naona mambo yalivyofanyika si sawa
alisema.
Askofu huyo ambaye huwa na msimamo usiotetereka, alisema tangu mwanzo zilifanyika mbinu ili rasimu hiyo ipitishwe, lakini wananchi ndio watakuwa waamuzi wa mwisho.
Wananchi wenyewe ndio watakuwa waamuzi wa mwisho, hatupaswi kuwa na magomvi yoyote, wananchi wana mamlaka ya kuamua kama wanaitaka hii Katiba au la
alisema.
Hata hivyo, askofu huyo alisema anaamini viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) watakutana kuzungumza na kushauri cha kufanya.

0 comments:

Chapisha Maoni