Jumatano, Oktoba 01, 2014

JAMAA ANYWA SUMU UKWENI TARIME, KISA KIKO HAPA

MFANYABIASHARA wa mjini Tarime mkoani Mara, Wilson Weso maarufu Kishimba (34) amekufa kwa kile alichodaiwa amekunywa sumu nyumbani kwa baba mkwe wake.
Inadaiwa alifanya hivyo nyumbani kwa baba mkwe, Chacha Sasita ambaye ni mkazi wa kijiji cha Rebu kata ya Turwa, kutokana na mgogoro na mke aliyemtoroka na kwenda jijini Mwanza na kumwachia watoto wawili.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Lazaro Mambosasa alisema kifo hicho kilitokea juzi.
Alifariki dunia kwa kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu
alisema kamanda.
Kwa mujibu wa kamanda, baada ya mke wa mfanyabiashara huyo kuondoka, alichukua watoto alioachiwa na kuwapeleka kwa baba mkwe kabla ya kunywa sumu.
Mwili wa marehemu uligunduliwa muda mchache na wakazi wa kijiji hicho cha Rebu ambapo askari wetu walifika na kuuchukua mwili huo na kuupeleka chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya kwa uchunguzi zaidi
alisema Kamanda huyo na kuongeza kwamba polisi inaendelea na uchunguzi.

0 comments:

Chapisha Maoni