Jumatano, Oktoba 08, 2014

HALIMA MDEE AACHILIWA KWA MDHAMANA

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee na wenzake wanane wanaokabiliwa na kosa la kufanya maandamano bila ya kibali na kukaidi amri halali ya jeshi la Polisi iliyowataka kutawanyika.
Wafuasi, wapenzi na wanachama cha Demokrasi na maendeleo wamefurika katika mahakama ya hakimu kazi kisuti huku wakionyesha ishara ya vidole viwili juu wakati taratibu za kuwadhamini washtakia hao chini ya hakimu mkazi mwandamizi Janeth Kayulenda zikiwa zinaendeleo, ambapo baada ya kukamilisha taratibu hizo waliruhusiwa na kupokewa na kundi la wanachama na mashabiki wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kushindikana kwa dhamana ya washtakiwa hapo oktoba 7 mwanasheria wa Chadema Bw.Peter Kibatala amesema hakukuwa na tatizo kwa upande wa washtakiwa pamoja na wadhamini na kusisitiza kilichokwamisha zoezi la uhakiki wa nyaraka za wadhamani linalofanywa kwa mujibu wa sheria na upande wa mashtaka.
Baada ya kutoka kwa dhamana mahakamani hapo kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapokuja kusikilizwa maelezo ya awali Oktoba 21 mwaka huu, washtakiwa hao waliandamana kwa magari huku wengine wakitembea kwa miguu kuelekea mahakao makuu ya chama hicho.

0 comments:

Chapisha Maoni