Jumatatu, Oktoba 20, 2014

FANYA MAMBO HAYA 10 KURAHISISHA MAISHA YAKO KAMA UNAISHI PEKE YAKO

1. Usalama
Unapokuwa unaishi peke yako jitahidi uchonge ufunguo na umkabidhi mtu unayemwamini sana na pia kumbuka kuzima swichi zote pindi unapomaliza kutumia.

2. Usafiri
Unapoanza au unapoamua kukaa peke yako basi tafuta eneo ambalo ni rahisi kufika kwa vyombo vya usafiri kwani maoneo yaliyo mbali na vyombo vya usafiri yatakufanya kuchoka na kujihisi mpweke sana.

3. Mapambo
Pamba nyumba yako katika namna ya kuvutia kiasi kwamba itakufanya uikumbuke kila muda unapokuwa haupo. Hii itasaidia kukufanya uwahi kurudi na pia itavutia hata wageni watakaokuja kukutembelea.

4. Tafuta mbinu mbadala
Vifaa vya usafi wa nyumba au kuosha kuosha vyombo hasa kwa wanaume ni kazi ngumu sana kwahiyo basi ukiwa na mbinu mbadala kama vile vifaa vya kuoshea vyombo na vingine vya usafi hurahisisha kazi kama hizo vitakufanya uzoee hari.  
 
5. Burudani
Chagua eneo la kuishi ambalo halina vishawishi kama kumbi za starehe, jenga mfumo mzuri wa kujiburudisha kama vile muziki na kuperuzi kwenye mtandao.

6. Manukato
Manukato (airfresh) yanayotengenezwa viwandani sio mazuri kwa afya hivyo basi panda aina ya mimea yenye harufu nzuri na ya asili ili kuweka mazingira yako ya mvuto na harufu ya kuvutia.
 
7. Mpangilio
Pangilia mali au vitu vyako kufuatana na uhitaji na chagua sehemu maalumu kwa kila kitu chako ili vyote viwe na mpangilio ulio mzuri na hii itakurahisishia kazi pindi unapotafuta vitu hivyo.
 
8. Usafi
Pangilia vitu vyako vizuri ili ikurahisishie katika kufanya usafi wa nyumba yako. Nyumba ikiwa na harufu mbaya au wadudu haivutii kabisa kuishi na pia ni chanzo cha maradhi.

9. Chakula
Unapokuwa unaishi peke yako kupika ni suala gumu mno lakini inatakiwa uwe unajipikia hii ni kutokana na kula mtaani ni gharama na si vizuri kwa afya. Hivyo jitahidi angalau uwe unapata muda wa kujipikia.

10. Upweke
Ili kukabiliana na upweke tumia muda unaokuwa huna kazi kusoma vitabu na pia kutafakari mambo mbalimbali ya maisha. Hii itakufanya usijione mpweke na utakuwa na furaha muda wote.

0 comments:

Chapisha Maoni