Ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa tishio kubwa duniani huku ikiripotiwa
kusabisha vifo vingi katika eneo la Afrika Magharibi umeingia nchini
Marekani ambapo mgonjwa wa kwanza ameripotiwa katika mji wa Dallas,
Texas.
Mgonjwa huyo anaelezwa kuwa ni mtu aliyepata maambukizi alipokuwa
nchini Liberia na aliingia Mareikani kabla ya kuonesha dalili za ugonjwa
huo.
Maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian
wamesema kuwa mgonjwa huyo ambaye jina lake halikutajwa ametengwa katika
hospitali hiyo.
Maafisa wa kitengo cha Afya cha Marekani wamewatoa hofu raia wa nchi
hiyo wakisema wanaamini kuwa wataudhibiti ugonjwa huo kabla haujasambaa.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000
wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka
Liberia.
0 comments:
Chapisha Maoni