STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' leo
anatarajiwa kupiga shoo ya nguvu kwenye ufunguzi rasmi wa shindano la
Big Brother Afrika 2014, nchini Afrika Kusini.
Diamond anatarajiwa kupamba shoo hiyo ya ufunguzi ambapo pia atakuwa
sambamba na mwanamuziki wa Nigeria, Davido watakapoimba wimbo wao wa
‘Number One Remix’.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kupiga shoo katika ufunguzi wa shindano hilo la BBA, awali alifanya hivyo katika msimu wa saba.
Shindano hilo la kila mwaka, linaloandaliwa na kampuni ya Multchoice,
msimu huu ni la 9, likijulikana kama ‘Big Brother Hotshots’
linashirikisha washiriki kutoka nchi 12 za bara la Afrika na mshindi
anatarajiwa kuondoka na kitita cha dola 300,000.
0 comments:
Chapisha Maoni