Jumatano, Oktoba 01, 2014

CWT IRINGA WAKOMALIA MADENI YAO

Ili kuwa na maendeleo kwa sekta ya elimu walimu Mkoani Iringa wameitaka serikali kuchukua hatua za utekelezaji wa madai yao ya kulipwa deni lao na kurudisha mfumo wao wa kuendelea kulipwa mafao yao katika hifadhi mbalimbali za jamii.
Hayo yamesemwa na umoja wa walimu (CWT) katika maandimisho ya kilele cha siku ya mwalimu duniani ambapo kwa Mkoa wa Iringa yamefanyika leo Oct 01,mwaka huuu katika uwanja wa Samola Manispaa na Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuiasa jamii kwa ujumla,serikali na wadau mbalimbali wa elimu kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya taifa letu.
Akihutubia katika maadhimisho hayo kwa niaba ya naibu waziri wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Tamisemi dtk.Kasimu Majaliwa ,Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Iringa Bw.Adamu Swai amesema serikali imesha kusanya changamoto zote zizazowakabili walimu na siku za hivi karibuni itatoa tamko la changamoto hizo.
Bw.Swai ameongeza kuwa serikali imeipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kuiweka iwe katika mpango wa mabadilliko makubwa sasa (BRN) na kuiongezea bajeti kwa ajili ya kuongeza utendaji kazi kwa walimu na kupambana na uhaba wa vifaa mbalimbali vya kufundushia.
Aidha amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia walimu wenye maambukizi ya Ukimwi,kufanya vikao vya mara kwa mara ili kudumisha mahusiano mazuri kazina baina ya walimu na taasisi nyingine aidha amewaasa walimu kutofautisha mambo ya kisiasa na taaluma yao.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Iringa Bw.Stanslaus Mhogole amesema licha ya walimu kukabiliwa na changamoto mbalimbali wameendelea na utendaji kazi wao wa kila siku hali iliyopelekea maendeleo katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na shule ya sekondari ya Igowole kuongoza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu.
Hata hivyo Mgeni rasmi Bw.Swai amesema maadhimisho hayo yanaenda kwa kauli mbiu ya “wekeza kwenye elimu kwa ajili ya maendeleo” ambapo kilele cha maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Oct 05, mwaka huu Mkoani Kagera.

0 comments:

Chapisha Maoni