Jumapili, Oktoba 05, 2014

BINTI AFUKUZWA NYUMBANI BAADA YA KUMPA PENZI MGANGA

Mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23), anadaiwa kufukuzwa nyumbani kwao kufuatia kuchanganywa na penzi la mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi aliyejulikana kwa jina moja la Zein.
Akizungumza mara baada ya kutimuliwa kwao, binti huyo ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake walezi maeneo ya Kariakoo jijini Dar alisimulia kwamba alifukuzwa kwao kwa sababu hakulala nyumbani siku moja wiki iliyopita na aliporudi wazazi wake walezi wakamtaka arudi alipotoka.

Baada ya kufukuzwa sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kuja kwa mpenzi wangu (Zein) maana ninampenda na siku si nyingi atanioa.
Mama na wajomba wameshakubaliana na uamuzi wangu isipokuwa baba tu
alisema binti huyo.
Alipotafutwa mganga huyo mwenye maskani yake Magomeni-Mwembechai, Dar, alisema kwamba ni kweli yupo na binti huyo na lengo lake ni kumuoa.

0 comments:

Chapisha Maoni