Mambo mengi duniani hutokea kwa sababu maalum, ndivyo pia ilivyotokea kwa mwanamuziki wa zamani wa Bongo Fleva nchini Tanzania Mike T a.k.a Mnyalu na wimbo wake 'Nitarudi' aliomshirikisha Michael Ross, soma hapa alichokisema kama nilivyomnukuu...
Nakumbuka ngoma hii kabla sijaiandika, nilikaa muda mrefu sana nikipigana na Maisha hapa Dar bila kwenda nyumbani kwetu Iringa kuwasalimia wazazi.Niliwazoesha wazazi wangu haiwezi kupita mwezi nilikuwa nakwenda kusalimia, ila nilikaa mwaka mzima bila kwenda ndipo mama yangu alikuwa analalamika sana juu yangu kuwa sipigi simu siendi home kuwatembelea ila hakujua kwanini iko hivyo.Ndipo nikachukua karamu na karatasi nikaandika nyimbo ili iwe rahisi kwake kusikiliza, marehemu Roy toka G-Records ndio alinipa beat hiyo na vocal nikafanyia kwa Bony (Mawingu Studio), na ni kwa mara ya kwanza Michael Ross alikuwa anaimba kiswahili.Bahati mbaya nyimbo yangu hii marehemu mama hakuiskia kwani ilipokwisha nae akawa amefariki dunia, nikiisikiliza huwa nabaki na neno NINGELIJUA but kazi ya MOLA
0 comments:
Chapisha Maoni