Wanajeshi nchini Somali wameidhibiti
milima ya Galgala kutoka kwa wapiganaji wa kundi la
Al-Shabaab,kulingana na utawala wa eneo hilo.
Wanamgambo hao walikuwa wakiidhibiti milima hiyo ya Kaskazini mwa taifa hilo kwa miaka kadhaa.
Waziri wa habari wa Puntland amesema kuwa kamanda wa Alshabaab katika eneo hilo alisalimu amri miezi minne iliopita.
Kundi
hilo linaloshirikiana na lile la Al-Qaeda lina makao yake makuu kusini
na katikati mwa somalia ambapo vikosi vya Umoja wa Afrika vinafanya
mashambulizi.
Abdiweli Hirsi Abdille,ambaye ni waziri wa habari wa
jimbo la kaskazini mashariki mwa Somalia Puntland amesema kuwa vikosi
vya serikali vimeliteka jimbo hilo la Glagala katika mashambulizi
yaliotekelezwa alfajiri.
Hatahivyo hakutoa maelezo yoyote kuhusu wafungwa ama waliojeruhiwa.
Lakini
kituo cha redio cha Al Furqan,kinachojulikana kwa kuwapendelea
wapiganaji wa Al-Shabaab kimeripoti kwamba magari mawili ya kijeshi
yaliharibiwa na wanajeshi 16 kuuawa.
Galgala ni eneo la kipekee la Puntland ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa Alshabaab.
Kamanda
wa Al-Shabaab katika eneo hilo Said Atom alijiunga na vikosi vya
serikali mwaka huu na kuwawacha wapiganaji wake katika jimbo la
Puntland.
Wapiganaji wa Al-Shabaab wamefurushwa kutoka miji mikuu
katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ,lakini bado wanadhibiti miji
midogo katika maeneo ya mashambani.
0 comments:
Chapisha Maoni