Jumanne, Septemba 02, 2014

YANGA KUPAMBANA NA WAKENYA KESHO

Timu ya Young Africans kesho itashuka kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kupambana na timu ya Thika United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom Septemba 20 mwaka huu.
Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa kipimo kizuri kwa kikosi cha mbrazil Marcio Maximo ambacho kimeshacheza michezo mitatu mpaka sasa ya kirafiki dhidi ya timu za Chipukizi FC, Shangani FC na KMKM zote za Ligi Kuu ya Zanzibara na kuibuka na ushindi kwa michezo yote.
Young Africans ambayo ina kikosi cha wachezaji 31 wakiwemo vijana sita kutoka kikosi cha cha U20 waliopandishwa itacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa chini ya kocha mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva ambao wote ni raia wa Brazil.
Mechi itarajiwa kucheza kuanzia majira ya saa 11:00 jioni kwa saaa za Afrika Mashariki ili kutoa fursa kwa wafanyakazi wa maofisini, taasisi mbalimbali waweze kuwahi na kushuhudia mchezo huo.
Viingilio vya mchezo huo ni:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Bluu & Kijanni Tshs 5,000/=
Tiketi zitaanza kuuzwa kesho saa 3:00 asubuhi katika eneo la Uwnaja wa Taifa.
Wanachama, wapenzi washabiki na wadau wa soka kwa ujumla mnaombwa kujitokeza kwa wing kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuja kuwashangilia vijana wakipeperusha bendera ya kijani na njano kutoka mitaa ya Twiga/Jangwani.

0 comments:

Chapisha Maoni