Jumanne, Septemba 02, 2014

SIFA 16 ZA RAIS ANAYETAKIWA 2015

Mwanasiasa mkongwe nchini, Cleopa David Msuya, ametaja sifa 16 za rais ajaye.  Msuya ambaye ni Makamu wa rais na Waziri Mkuu Mstaafu, alisema kuwa sifa hizo ni muhimu kwa ustawi wa taifa.
Msuya alizitaja sifa hizo kuwa ni uadilifu, uzalendo, mpambanaji na jasiri dhidi ya rushwa na ufisadi na mwelewa na msimamizi wa uchumi.Alitaja nyingine kuwa ni ustawishaji wa uchumi sawia (economic equity and fair distribution of income and other economic benefits) na awe na uelewa wa kujua umuhimu wa kujenga na kusambaza sawia huduma za miundombinu ya kiuchumi na kijamii.
Sifa ya saba aliitaja kuwa ni mtu mwenye kujua umuhimu wa watu kufanya kazi, nane awe na uwezo wa kuwatetea na kukomesha unyanyasaji wa wananchi ndani ya nchi yao, tisa uwezo wa kuelewa misingi ya uchumi wa taifa na 10 awe na uwezo wa kufumua maovu na machafu yanayofanyika. Sifa ya 11 ni kuwa mnyenyekevu na mapenzi kwa taifa na wananchi, sifa ya 12 awe na uwezo kuongoza na kuona mbele, sifa ya 13 awe na uwezo wa kutofautisha mambo ya nchi na binafsi.
Msuya ametaja sifa ya 14 kuwa ni kutofautisha mambo ya biashara na mali za umma, 15 kutofautisha mambo ya ofisi na nyumbani na sifa ya 16 ni mwenye uwezo wa kusimamia na kuwezesha wananchi katika uchumi. Kiongozi huyo ambaye alipata kushika nafasi ya Waziri Mkuu kwa vipindi viwili tofauti chini ya Mwalimu Nyerere na baadaye chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, aliainisha kila sifa kwa maelezo ya kina kuashiria kuwa huko tuendako taifa linahitaji kuwa makini sana katika kuchagua viongozi.
Awe na sifa ya uadilifu usio na shaka na Watanzania wamfahamu na kumwelewa kuwa ni kiongozi anayefahamika na kueleweka na wananchi kuwa ni mwadilifu wa
kiwango cha juu kabisa
alisema akifafanua kwa kina maana ya sifa ya kwanza.

0 comments:

Chapisha Maoni