Jumatano, Septemba 17, 2014

WATU WA SCOTLAND KUPIGA KURA YA KUJITENGA NA UINGEREZA LEO

Wakazi wa eneo la Scotland leo wataelekea katika masanduku ya kupigia kura ili kushiriki katika kura ya maoni kwa ajili ya kuamua iwapo watajitenga na Uingereza au la.
Hatua hiyo inaweza kuandaa mazingira ya eneo hilo la Ulaya kujitawala lenyewe na kuwa taifa changa zaidi barani humo hapo baadaye. Wakati wa kampeni za kura hiyo ya maoni, kambi zote mbili za 'ndio' na 'hapana' zilivutia upande wake, huku baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Uingereza wakiwatia hofu watu kwamba, kujitenga kutasababisha matatizo ya kiuchumi kwa Scotland hapo baadaye.
Hata hivyo maafisa wa Scotland wanasema kuwa, kujitenga eneo hilo kutoka Uingereza kutawaepusha wakazi wake na siasa za kubana matumizi za London na pia gharama za kijeshi zisizo na lazima.
Zaidi ya watu milioni 4 wamejiandikisha kupiga kura, huku matokeo ya uchunguzi wa maoni yakionesha kuwa, idadi ya wanaopinga na wanaoafiki kujitenga inakaribiana.

0 comments:

Chapisha Maoni