Katika hali isiyokuwa ya kawaida Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki
Jimbo Kuu la Dar es Salaam Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji
Luhanga, Padri Richard D’souza, ameshindwa kufungisha ndoa baada ya bibi
harusi kubainika kuwa ni mke wa mtu.
Bibi harusi aliyejulikana kwa jina la Neema Hoza, ambaye alitaka
kufunga ndoa na mwanamme mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana
mara moja, anadaiwa kuwa alishafunga ndoa na Brighton Mhache katika
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kimara.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,
kaka wa mume wa Neema, Fadhili Mhache, alisema mdogo wake
alikwishafunga ndoa na Neema, lakini cha kushangaza shemeji yake huyo
kutaka kufunga ndoa tena wakati kikanisa hairuhusiwi.
Mhache, alisema walifikia hatua hiyo ya kwenda kanisani kusimamisha
ndoa hiyo, kwa sababu Neema alikuwa bado ni mke wa mtu, hivyo
hakustahili kuolewa na mwanamme mwingine na kwamba, aliondoka nyumbani
akisema anakwenda kwa dada yake kupumzika.
0 comments:
Chapisha Maoni