Jumatatu, Septemba 01, 2014

MSIGWA: MUWAJALI WALEMAVU NA KUWAPA FURSA

Wananchi na viongozi wa serikali na asasi za kiserikali pamoja na zisizo za kiserikali Mkoani Iringa wametakiwa kuwajari walemavu kwa kuwapa fursa za kushiriki katika ngazi za uongozi na kazi mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh.mch.Peter Msigwa ameyasema hayo katika mkutano na hafla ya chakula cha pamoja na walemavu ambapo lengo kuu lilikuwa ni kuzitambua changamoto zinazowakumba walemavu hao.
Kwa upande wa walemavu wa ngozi wamesikitishwana na kuibuka kwa vitendo vya mauaji ya albino,kunyanyapaliwa kwa kutengwa na kuitwa majina ya zeruzeru na dili,kukosa mafuta maalumu kwa matibabu ya ngozi pamoja na wanafunzi kutokuwa na vifaa maalumu yakiwemo miwani ili kupata urahisi wa kusoma.
Aidha walemavu wa miguu na viziwi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kukosa ajira licha ya kuwa na elimu,miundo mbinu isiyo rafiki kwao katika barabara, maeneo ya huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madirisha kwenye maeneo ya mapokezi ya huduma hizo.
Hata hivyo Mbunge Msigwa amewataka walemavu wenye uwezo wa kuFanya kazi kujiingiza kwenye shughuli za uzalishaji mali na kuachana na vitendo vya kuwa ombaomba hivyo ameahidi kushirikiana na viongozi husika wa taasisi mbalimbali kujenga miundo mbinu kwa ajili ya makundi maalumu ya walemavu.

0 comments:

Chapisha Maoni