Jumanne, Septemba 02, 2014

MEYA KAPUNGA AWACHEFUA MASHABIKI WA MBEYA CITY

Katika mazingira yasiyotarajiwa, Meya wa jiji la Mbeya, Athanus Kapunga, mwishoni mwa wiki alijikuta katika wakati mgumu akishindwa kuhutubia baada ya mashabiki wa soka kuanza kuzomea wakikerwa na hatua yake ya kuingiza masuala ya siasa katika hafla hiyo michezo.
Hiyo ilikuwa katika hafla ya Siku Familia ambayo ilifanyika Uwanja wa Sokoine, ikitumika pia umtambulisha kocha Msaidizi wa timu hiyo, Selemani Mahmoud Jabri ambapo Meya huyo, aliwakera wapenzi na mashabiki wa soka kwa kitendo chake cha kuingiza masuala ya siasa.
Baada ya kupewa kipaza sauti na msheheshaji wa hala hiyo, Chareles Mwakiupesile, aweza kutoa salamu kwa umati uliofurika uwanjani hapo na kumkabisha mgeni rasmi, Kapunga alisema uwepo wa timu hiyo ni utekelezaji wa ilani ya CCM, kauli ambayo iliwakera wengi ambao walianza kuzomea na kuzusha vurugu kwa takribani dakika kama 10
Akifafanua zaidi juu harakati za kuanzisha timu hiyo, Kapunga alisema ni baada ya kupokea mawazo kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji hilo, Juma Idd alijaribu kupitia ilani ya chama chake na kujiridhisha kuna suala la michezo, hivyo akapeleka wazo hilo katika Baraza la Madiwani.
Source: Tanzania Daima

0 comments:

Chapisha Maoni