Jumanne, Septemba 02, 2014

JUSTIN BIEBER AZUA TENA

Justin Bieber ameshtakiwa kwa kushambulia mtu na kwa uendeshaji hatari baada ya kugonga gari akiwa anaendesha pikipiki yake ya matairi manne. Alikamatwa karibu na mji aliozaliwa wa Stratford, Ontario, baada ya kuanza kupigana na dereva wa gari aliloligonga. Polisi wa Ontario wamethibitisha kuwa waliitwa katika eneo la tukio kuchunguza na wamekamata mtu. Polisi baadaye walimuachilia huru katika kile kijulikanacho kama "ahadi ya kurudi tena" mahakamani Septemba 29. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, uchunguzi "umeonesha kuwa baada ya ajali hiyo kutokea, dereva wa gari na wa pikipiki 'walikunjana' mashati"

0 comments:

Chapisha Maoni