Jumatano, Septemba 03, 2014

2 WAFA IRINGA KATIKA AJALI 2 TOFAUTI

Watu wawili wamefariki Mkoani Iringa katika matukio mawili ya ajari za barabarani huku jeshi la polisi likiwatafuta madereva wawili ambao wamekimbia baada ya kusababisha ajali hizo.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema mtoto Augustino Kisumbe umri miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Lyasa Wilaya ya kilolo Mkoani Iringa amefariki papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki ambayo ilikuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika jina wala makazi yake.
Ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea barabara kuu ya Ilula-Image,chanzo chake kikiwa ni mwendo kasi ambapo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumtafuta dereva aliyesababisha tukio hilo.
Kamanda Mungi amesema John Mwendisile umri wa miaka 57 akiwa anaendesha baiskeli yake maeneo ya Ikuvilo wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa amefariki papo hapo baada ya kugongwa kwa pikipiki T:510 CNP aina ya Boxer ikiendeshwa na dereva asiyefahamika jina wala makazi yake.
Aidha amesema ajali hiyo imetokea barabara kuu ya Ugwachanya-Ikuvilo,chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa mwendesha baiskeli na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kumtafuta dereva wa pikipiki.
Hata hivyo Kamanda Mungi ametoa wito kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni