WATU wawili wamekufa baada ya gari la Kijeshi (Kifaru cha Jeshi la
Wananchi Tanzania JWTZ) kupoteza mwelekeo na kuparamia makazi ya watu
mkoani Lindi na kupelekea watu wengine saba kujeruhiwa vibaya.
Taarifa zilizoifikia Fichuo Tz muda huu na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani humo zinaeleza kuwa
ajali hiyo imetokea saa 05:30 asubuhi katika eneo la Mnonela barabara ya
Mingoyo-Mtwara na kuwa ajali hiyo ilihusisha gari namba 018 APC mali ya
JWTZ kikosi namba 83 Reget.
Gari hilo lilikuwa likitokea mkoani Mtwara kuelekea katika wilaya ya
Nachingwe mkoani Lindi kikazi ambapo lilikuwa likiendeshwa na Askari
mwenye namba MT 99241 Priv. Shadhil Nandonde pia haijawekwa wazi kuwa ni
kazi gani lilikuwa linaenda kufanya shughuli gani.
Imeelezwa kuwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Askari
mwenye namba MT 10728 Pr Pascal Komba na mwanamke aliyetambuliwa kwa
jina la Somoe Kamtaule (75), mkulima wa eneo hilo aliyekuwa ndani ya
nyumba.
Lilipoteza mwelekeo na kuingia kwenye nyumba mbili na katika nyumba moja ilisababisha kifo cha mtu mmoja (mwanamke) na kwenye gari hilo Mwanajeshi mmoja alikufa pamoja na majeruhi saba kujeruhiwa vibaya
Aidha, majeruhi katika ajali hiyo ni Askari mwenye namba MT 10744 Pr.
Simon Edward, Askari namba MT 106842 Pr.Feruz Haji, Askari mwenye namba
MT 1077263 Pr.Omary Makao pamoja na Askari mwenye namba MT 99018
Pr.Mbaruk Duchi.
Wengine ni Askari mwenye namba MT 107442 Pr. Simon Masele, Askari mwenye
namba MT 107218 Pr.Ndekenya R na Askari mwenye namba MT 99241
Pr.Shadhil Nandonde ambaye alikuwa dereva.
Kwa mujibu wa Polisi mkoani humo, chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na
majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mtwara ya
Ligula kwa ajili ya matibabu.




0 comments:
Chapisha Maoni