Wizara ya Uchukuzi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imetangaza
leo kuwa, kwa kiasi cha watu 80 hawajulikani walipo, baada ya boti
waliyokuwa wamepanda kuzama katika Mto M'poko ulioko kusini mwa nchi
hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya Jamhuri ya Afrika ya
Kati imeeleza kuwa, boti hiyo ilibeba zaidi ya watu 100, ambapo watu 50
kati yao waliokolewa na wengine wasiopungua 80 hawajulikani walipo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kuzama kwa boti katika Mto M'poko limekuwa
jambo la kawaida, kwani vyombo hivyo vya baharini vinapakia watu na
mizigo kupita kiasi.
Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini
na ardhi ya kilimo, inakabiliwa na matatizo makubwa katika sekta ya
miundombinu na lindi la umasikini.
0 comments:
Chapisha Maoni