Jumatano, Agosti 13, 2014

WALICHOSHAURIWA WAKULIMA WA IRINGA

Wakulima Mkoani Iringa wameshauriwa kuandaa mashamba vizuri kabla ya kulima na kutafuta pembejeo bora ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bibi. Rose Kasole amesema, maandalizi mazuri ya shamba huongeza uzalishaji bora hali ambayo itasaidia kuongeza kipato cha mkulima.
Bibi. Kasole amewakumbusha wakulima kutambua nyakati za kilimo kwa kupanda mazao yao kipindi cha mvua za mwanzo ili kuongeza uzalishaji wa mazao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha, amewashauri wakulima kuwa na mipango mikakati ya kilimo hali ambayo itawasaidia kuzalisha kwa ufanisi na kuwaingizia kipato zaidi.
Bi Kasole ameongeza kuwa ongezeko la mardhi ya utapia mlo na udumavu katika mkoa wa Iringa hutokana na ardhi kukokasa madini ya Iodine (Ayodini) katika mazao yanayolimwa kwa sababu ya hali ya baridi.
Hata hivyo, Afisa Kilimo huyo amewashauri wakulima kuwatembelea maafisa kilimo wa vijiji na kata ili kuapata elimu ya kilimo bora ikiwemo matumizi ya pembejeo bora za mbolea na mbegu.

0 comments:

Chapisha Maoni