Alhamisi, Agosti 28, 2014

WAKAMATWA NA SHORTGUN IRINGA

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikiria watu wawili kwa tuhuma za kumiliki silaha‭ ‬aina ya shortgun yenye risasi nne kinyume cha‭ ‬sharia‭ ‬za nchi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP.‭ ‬Ramadhani Mungi amesema,‭ ‬watuhumiwa hao‭ ‬Juma Kwike miaka‭ ‬38‭ ‬na Gerard Sulime‭ ‬miaka‭ ‬42‭ ‬wote wakazi wa wilayani Kilolo,‭ ‬mkoani Iringa.
Kamanda Mungi amemeongeza kuwa,‭ ‬jeshi la polisi‭ ‬limewakamata‭ ‬watuhumiwa hao wakiwa kwenye doria katika‭ ‬eneo la‭ ‬kijiji cha Ifuha,‭ ‬kata ya‭ ‬Udekwa,‭ ‬tarafa ya‭ ‬Mahenge,‭ ‬mkoani Iringa.
Hata hivyo,‭ ‬kamanda wa‭ ‬polisi‭ ‬mkoani Iringa amesema,‭ ‬jeshi lake linaendelea‭ ‬kufanya uchunguzi‭ ‬zaidi ili‭ ‬kubaini umiliki‭ ‬wa silaha‭ ‬hizo kwa watuhumiwa.

0 comments:

Chapisha Maoni