Jumanne, Agosti 19, 2014

VETA NYANDA ZA JUU KUSINI IMEAMKA...UKAGUZI KUFANYIKA

Usajili wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwenye eneo la Nyanda za Juu Kusini unaweza kusaidia kutoa elimu yenye kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Mratibu wa VETA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. John Mwanja amesema, kuna vyuo ambavyo havijasajiliwa ambavyo vinaleta usumbufu.
Bw. Mwanja amesema, wameanza kuzunguka kwenye maeneo mbalimbali ili kuwaelimisha wamiliki na wananchi wenyewe.
Aidha amesema wamiliki wa vyuo wanatakiwa kutambua, wazazi wanaowapeleka watoto wao wanalengo la kuwasaidia katika suala la ajira.
Hata hivyo, mratibu huyo ameishauri jamii kuepukana na mtazamo wa masomo ya vyuo vya VETA kama ni kwa ajili ya watu wenye kukosa ufaulu mzuri bali ni kwa ajili ya watu wote.

0 comments:

Chapisha Maoni