Alhamisi, Agosti 21, 2014

USHAURI WAKO TAFADHALI

Habari zenu wasomaji wa Fichuo! Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 30 Naishi mombasa ila ni mzaliwa wa mbeya nchini Tanzania. Nimejitokeza kwenu kushare tatazo langu linalo nitesa sana moyoni, Mimi nilikua na mpenzi wangu ambea tulikutana chuo pale Tumaini mkoani iringa kiukweri nilimpenda sana mpenzi wangu lakini kwakua mapenzi hayana huruma huwezi amini kilicho tokea kwanza kabisa mpenzi wangu aliniomba nimfungulie duka mamaake mzazi mimi kwakua nilimpenda sana sikuona ugumu wowote kwake nilimfungulia duka mamaake na nikampa mtaji wa kutosha kabisa. Nilivyo maliza chuo kuna wa zungu waliniomba twende wote mombasa ili nikajiendeleze kielimu mimi niliwakubalia pia nikamueleza mpenzi wangu akanielewa. Chaajabu kilichotoke mwezi uliopita nimerudi Tanzania nimemkuta mpenzi wangu anamimba ya rafiki yangu wa damu sio sili imeniuma sana pale alivyo nambia alie mpa mimba kamkana anaomba nimsamehe nilee mimba hawezi rudia tena kunisaliti. Sasa naombeni ushauri wenu wadau nifanyeje hapa nilee mimba au niachane nae?

0 comments:

Chapisha Maoni