Rapper wa Young Money, Tyga na mrembo Blac Chyna aliyekuwa stripper
wamepigana chini ikiwa ni miaka mitatu tangu walipoanza safari ya penzi
lao.
Kwa mujibu wa TMZ, Tyga ameachana na msichana huyo ambaye wamezaa nae
mtoto wa kiume lakini bado kuna utata kuwa mrembo huyo amegoma kutoa
vitu vyake katika nyumba ya Tyga.
Tyga alikosolewa sana na kutabiriwa mwisho mbaya baada ya kuamua
kumchukua Blac Chyna katika club maarufu ya wasichana wanaocheza wakiwa
watupu.
Wawili hao walikutana mwaka 2011 katika party ya Chris Brown na kutengeneza couple ambayo ilikuwa maarufu.




0 comments:
Chapisha Maoni