Ambwene Yesaya ‘AY’ ameanika siri za Ikulu ya Rais Baraka Obama wa
Marekani, baada ya kuitembelea wakati alipokwenda kwa ajili ya shoo
akiwa na wenzake tisa kutoka Afrika.
Nilipokwenda sikumkuta Rais Obama, alikuwa Minnesota kwa mambo yake, lakini tulipokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ed Royce ambaye pia alihudhuria shoo yetu. Pale tulipewa ‘brief’ kidogo na mambo mengine yakaendelea
alisema AY.
Alisema wakati wa mazungumzo yake na Royce, kiongozi huyo alimwambia
Marekani imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa viongozi wa Afrika, lakini
zinatumika ndivyo sivyo, hivyo hivi sasa inafikiria kubadili uelekeo ili
iwe inatoa msaada zaidi kwa wasanii wakiamini wanaweza kufikia malengo
yao.
Alisema pia alipata muda wa kubadilishana mawazo na mabosi wa Benki ya Dunia na wale wa shirika la misaada la Marekani, USAID.
Alisema pia alipata muda wa kubadilishana mawazo na mabosi wa Benki ya Dunia na wale wa shirika la misaada la Marekani, USAID.
Katika
shoo yao iliyofanyika New Seum, Washington, DC, watu mbalimbali
walihudhuria akiwemo nyota wa muziki wa Afrika mwenyeji wa Senegal,
Akon.AY alikuwa mmoja wa wasanii hao tisa waliochaguliwa kutoka nchi 11
za Afrika, waliokwenda katika ziara hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati
ya Ikulu ya Marekani na shirika la One Organization.



0 comments:
Chapisha Maoni