Rapper T.I anakabiriwa na kesi ya wizi wa vifaa vya jukwaani
ambavyo alivikodi mwaka jana wakati wa Tour ya America’s Most Wanted
aliyofaya na Lil Wayne na rappers wengine.
Kwa mujibu waTMZ, kampuni iliyomkodishia vifaa hivyo imeeleza katika
shitaka lake kuwa ilimkodishia vifaa T.I na akalipia gharama za
kukodisha lakini wakati wa kurudisha hakurudisha Screen ya gharama
kubwa inayofahamika kama Roll Drop inayotumika kuonesha picha na video
wakati wa show.
Screen hiyo imetajwa kuwa na thamani ya $50,000 lakini kampuni hiyo
inataka T.I ailipe $100,000 kwa kuwa katika muda wote iliyopotea
ingekuwa imewaingizia kiasi hicho cha pesa kwa kuwakodishia watu
wengine.
Tuhuma hizo zinakuja wakati ambapo T.I anaendelea kupiga kazi ya
kuandaa albam yake mpya inayoitwa ‘Paperwork: The Motion Picture.
T.I ameeleza katika mahojiano alioyofanya hivi karibuni kuwa albam
hiyo itawashikirisha Rick Ross, The Dream, Lil Boosie, Young Jeezy na
wengine wengi.
Bado tarehe rasmi ya kutoka haijapangwa.
0 comments:
Chapisha Maoni