Jumatatu, Agosti 18, 2014

NENO ALILOTUMIA DRAKE 'YOLO' LAINGIZWA KATIKA KAMUSI YA OXFORD NA KUZUA UTATA

Kamusi ya kiingereza ya Oxford (Oxford Dictionary) imeingiza rasmi kwenye catalog yake ya online msemo anaopenda kuutumia Drake ‘YOLO’.
Msemo huo ambao ni herufi nne zinazoelezea ufupisho wa neno ‘We All Live Once’ unakuwa miongoni mwa Phrases kama vile FML, SMH na maneno mengine ambayo sio ya ufupisho.
Drake alilitumia ‘YOLO’ kwa mara ya kwanza mwaka 2011 katika wimbo wake The Motto uliokuwa kwenye albam ya Take Care.
Hata hivyo wadau wengi wamekosoa kuwa Drake sio mtu wa kwanza kulitumia neno hilo bali yeye amesaidia kulipatia umaarufu zaidi. hivyo hapaswi kuchukuliwa kama mmiliki wa YOLO.
Wameonesha sehemu 11 ambazo neno hilo lilitumika sana ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwenye filamu tena likiwa na maana hiyo hiyo. Hizi ni baadhi tu. Hii inadaiwa kutumika mwaka 1939.

0 comments:

Chapisha Maoni