Alhamisi, Agosti 28, 2014

TETESI ZA USAJILI ULAYA KATIKA SIKU 4 ZILIZOSALIA

Boss wa Manchester United Louis van Gaal anajaribu kumnunua kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, na beki wa Ajax Daley Blind, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba mosi (Daily Mirror), United watalazimika kulipa pauni milioni 20 kumsajili Blind (Sun), Liverpool bado wanajaribu kumfuatilia kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ambaye yuko Barcelona (Metro), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hatotaka kuwasajili Danny Welbeck, 23, kutoka Man U, Radamel Falcao kutoka Monaco, 28, na Nikola Zigic, 33, kutoka Birmingham (London24.com), Manchester United watapanda dau la pauni milioni 24 kwa kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22, wakati Louis van Gaal akitaka kuwaondoa Welbeck, Tom Cleverly, 25, na Shinji Kagawa, 25 (Daily Telegraph), Cleverly yuko tayari kusalia hadi mwaka ujao mkataba wake utakapokwisha (Independent), Sunderland wametoa dau la pauni milioni 6 kumsajili beki Virgil van Dijk, 23, kutoka Celtic baada ya Toby Alderweireld, 25 wa Atletico Madrid kukataa kwenda kuichezea Black Cats (Times), mchezaji wa zamani wa Juventus Allesandro Del Piero amekubali kujiunga na Delhi Dynamos ya India baada ya mkataba wake na Sudney FC kumalizika (Football Italia), Crystal Palace wanajiandaa kumsajili tena Wilfried Zaha kutoka Manchester United baada ya Neil Warnock kurejea kama meneja (Daily Star), kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso, 32 anakaribia kujiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa pauni milioni 8 (Guardian), Real Madrid wanataka kumsajili Marco Reus lakini wapo tayari kusubiri hadi msimu ujao (AS), Chelsea wamekubali euro milioni 12.5 kutoka AC Milan kumsajili Fernando Torres (The Sun), Borussia Dortmund wameonesha nia ya kumrejesha Shinji Kagawa katika Bundesliga, baada ya kushindwa kuwika akiwa Old Trafford (Kicker), maafisa wa Juventus wamekutana na maafisa wa Monaco kujadili suala la Radamel Falcao kwa mkopo (Gazetta dello Sport), Inter Milan wanataka kumchukua Xherdan Shaqiri kutoka Bayern Munich, iwapo Ricky Alvarez ataondoka wiki hii kwenda Sunderland (Corriere dello Sport) Diego Costa huenda akakosa kucheza kwa wiki sita baada ya kuumia msuli wa paja (Daily Telegraph). Zimesalia siku nne kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

0 comments:

Chapisha Maoni