Jumanne, Agosti 12, 2014

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI YA ULAYA

Beki wa Liverpool Kolo Toure, 33, anajiandaa kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki katika mkataba wa pauni milioni 1.5 (Daily Mail), boss wa Liverpool Brendan Rodgers anafikiria kumchukua mshambuliaji kutoka Cameroon, Samuel Eto'o, 33, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea msimu uliopita (Guardian), Galatasaray wanafikiria kutoa pauni milioni 28 kuwachukua Joel Campbell, 22, na Lukas Podolski, 29, kutoka Arsenal (Daily Express), QPR wapo tayari kumtoa Loic Remy, 27, kubadilishana na Andros Townsend, 23, na Harry Kane, 21 kutoka Tottenham (CaughtOffside), Remy pia huenda akawindwa na Chelsea, wakati Jose Mourinho akitafuta mchezaji wa kuziba pengo la Didier Drogba, 36, aliyeumia (Goal), kiungo kutoka Spain Santi Cazorla, 29, ametupilia mbali tetesi kuwa anataka kuondoka Arsenal na kurejea La Liga (Daily Mirror), Stoke City wamepanda dau jipya na kutoa pauni milioni 5 kutaka kumchukua winga wa Norwich Nathan Redmond, 20 (Daily Mail), Aston Villa wanakaribia kumchukua Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 3.5 (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba huenda asiweze kucheza kwa miezi minne baada ya kuumia 'enka' katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ferencvaros (Daily Mirror), Southampton huenda wakampiga faini Morgan Schneiderlin, 24, iwapo kiungo huyo Mfaransa atakataa kucheza mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili (Daily Telegraph), kipa wa Manchester City Willy Caballero, 32 amemwambia kipa mwenzake Joe Hart, 27, atalazimika kupigania namba moja, Etihad (Telegraph), Chelsea wanamfuatilia beki wa kati wa Roma, Mehdi Benatia, 27, ambaye anadhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30 (Daily Mirror), Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 10 kumshawishi beki wa kati wa Liverpool Daniel Agger (The Sun), Everton na Tottenham wako 'macho' baada ya kuambiwa Salomon Kalou anaweza kuondoka Lille kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Daily Mirror), Arsenal wapo tayari kumfuatilia beki wa Olympiakos Kostas Manolas kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Daily Express).

0 comments:

Chapisha Maoni