Siku kama ya leo miaka 166 iliyopita aliaga dunia George Stephenson
raia wa Uingereza na mbunifu wa Locomotive yaani kichwa cha gari moshi.
Alizaliwa mwaka 1781. Stephenson alipenda sana masuala ya ufundi na
alipata mafunzo katika nyanja mbalimbali za ufundi na hisabati. Baada ya
hapo George Stephenson alifanikiwa kutengeneza chombo muhimu cha
uchukuzi na usafirishaji yaani Locomotive au kichwa cha gari moshi.
Locomotive hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa na
ilikuwa na uwezo wa kubeba uzito wa tani 90. Baadaye iliongezewa kasi na
uwezo wa kubeba mizigo.
Tarehe 12 Agosti mwaka 1949 hati ya makubaliano ya kimataifa ya
kuwalinda majeruhi na mateka wa kivita ilipasishwa kwenye makao makuu ya
Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi. Hati hiyo ilibuniwa kufuatia
miamala isiyo ya kibinadamu na jinai zilizokuwa zikifanywa dhidi ya
majeruhi na mateka wa kivita wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Na siku kama hii ya leo miaka 38 iliyopita sawa na tarehe 12 Agosti
1976, kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Tel al Zaatar iliyoko karibu na
Beirut mji mkuu wa Lebanon, ilitekwa baada ya kuzingirwa kwa muda mrefu
na wanamgambo wa Kimaroni wa nchi hiyo na wakazi wake wakauawa kwa
umati. Kambi hiyo ilikuwa ikiwahifadhi maelfu ya wakimbizi wa Palestina
na ilianza kuzingirwa mwanzoni mwa mwaka 1976 kwa uungaji mkono na
uingiliaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Utawala wa Kizayuni
ulifanya hivyo kwa lengo la kushadidisha vita vya ndani huko Lebanon.
0 comments:
Chapisha Maoni