Rubani mmoja nchini Uingereza alipoteza mwelekeo
angani akiendesha ndege ya biria baada ya mkono wake wa bandia kuchomoka
wakati alipokua akielekea kutua.
Rubani huyo wa shirika la ndege la Flybe mwenye
umri wa miaka 46 , aliruka kutoka uwanja wa ndege wa Birmingham, akiwa
na abiria wapatao 47 ndani yake, wakati alipokaribia kutua katika uwanja
wa ndege wa mji wa Belfast alikumbana na upepo mkali angani ambao
ulimsababisha atue kwa ghafla ilivyo bahati hakukuwa na madhara kwa
ndege yenyewe wala abiria.
Katika maelezo aliyoyatoa baada ya
manusura, mkurugenzi wa shirika hilo la ndege la Flybe Captain Ian
Baston, anayehusika pia na masuala ya usalama katika shirika hilo la
Flybe alimuelezea rubani kiongozi wa ndege hiyo aliyekua akiiongoza kuwa
ni mwenye uzoefu wa hali ya juu na mwenye kuaminiwa pindi awapo angani,
na hivyo usalama wa abiria na wahudumu huwa katika mikono iliyo salama
sana .
Muda mfupi tu kabla ya kuielekeza ndege Dash 8
kutua kwa dharula rubani huyo alijikagua na kuona kwamba mkono wake
bandia wa shoto ulikua sawa lakini baada ya tukio hilo ghafla akajikuta
mkono huo umechomoka.
Ndege hiyo ilitua kwa mlio mkubwa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa na pia ndege haikuharibika.
Rubani alisema atakuwa makini zaidi katika siku za usoni kuhusiana na mkono wake huo bandia.
0 comments:
Chapisha Maoni