Ijumaa, Agosti 15, 2014

MMILIKI WA FACEBOOK AMWAGIA BARAFU BIL GATES

Huko Marekani na Canada kuna kampeni maalum inayoendelea ya kuchangia matibabu na elimu ya ugonjwa wa ALS (Amyotrophic lateral sclerosis au Lou Gehrig’s disease) ambao umekuwa tishio kwa watu wengi.
Kampeni hiyo inafanyika kwa kuhamasisha watu maarufu au matajiri kuchangia na kuonesha ishara kwa ndoo ya maji ya barafu kichwani kama ishara ya kuunga mkono kampeni hiyo na kisha kuwataja watu watatu ambao unawachallenge na kuwataka wachangie pia kama wewe.
Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerbrg ameamua kujimwagia ndoo ya barafu baada ya kutajwa na matajiri wenzake. Na yeye baada ya kufanya hivyo amempasia kijiti hicho kwa Bill Gates kuwa naye ajipige ndoo ya barafu na kuchangia. Wengine aliowataja ni Sheryl Sandberg na Reed Hastings.
Kampeni hiyo inafanikiwa kwa kiasi kikubwa sasa na endapo Bill Gates na hao aliowataja wakifanya hivyo pia mfuko huo unategemea kutuna kwa kiasi cha kutosha.
ALS ni ugonjwa ambao humshambulia mtu na kudhoofisha misuli hivyo mwili mzima huishiwa nguvu kabisa.

0 comments:

Chapisha Maoni