Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuwawa kikatili
kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika katika eno la
mkundi manispa a ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema
wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha
kumwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi
kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.
Wananchi wakazi wakata ya mkundi wamesema hilo sio tukio la kwanza
kutoke kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya
sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu
kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru
na vyombo vya sheria pasipo kuchukuiwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kw atukio hilo na limefika katika eno la tukio.
0 comments:
Chapisha Maoni