Wakati bunge la katiba likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma baadhi
ya wananchi Songea vijijini hawajawahi kuiona katiba na hawajui
inazungumzia nini huku wanaharakati mkoani Ruvuma wakitaka kufanyike
maridhiano ya pande zote mbili kwa kuwa haiwezi kupatikana katiba ya
upande mmoja.
Hayo yamebainika katika mdahalo wa katiba ulioandaliwa na shirika
la Restles Development na kufanyika mpandangindo Songea vijijini mkoani
Ruvuma ambao umekuwa ukihusiana na haki za wanawake katika katiba mpya
na kuwaandaa wananchi kuipigia kura katiba itakayopitishwa na bunge la
katiba ili iwe katiba kamili.
Kufuatia hali hiyo mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali
yamekuwa yakiendelea kutoa elimu ya katiba kwa wananchi licha ya
midahalo hiyo kupigwa vita na baadhi ya viongozi wa serikali ambapo
wananchi wamekuwa wakishukuru kwa kupatiwa elimu hiyo.
Kwa upande wake mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto mkoani
Ruvuma Bi. Anna Tembo ametoa wito kufanyike mardhiano kati ya pande
mbili zinazosigana ili iweze kupatikana katiba mpya kwa kuwa haiwezi
kupatikana katiba ya upande mmoja.
0 comments:
Chapisha Maoni