Wakati Michael Jackson akiwa amelala kwenye nyumba yake ya milele,
bado familia yake imeendelea kuandamwa na tuhuma nzito zinazomhusu
mfalme huyo wa Pop duniani.
Mlalamikaji, James Safechuck mwenye umri wa miaka 36 hivi sasa ambaye
alikuwa katika kesi ya Michael Jackson ya mwaka 2005 kuhusu ulawiti,
ameibuka tena na kufungua kesi na kutoa ushahidi mpya wa jinsi
alivyokuwa akilawitiwa na marehemu mwaka 1988 wakati akiwa mtoto mwenye
umri wa miaka 10 tu.
James ambaye sasa ni baba wa familia hakuonesha ushirikiano wakati wa
kesi ya mwaka 2005 licha ya kutajwa kama sehemu ya ushahidi.
TMZ wameeleza kuwa wamepata nyaraka zilizowasilishwa na Safechuck
mahakamani ambazo zinaeleza kuwa Michael Jackson alimfundisha lugha ya
ishara wakati akiwa na umri wa miaka kumi, lugha ambayo alikuwa
akiitumia kutaka kumueleza kuwa anataka kufanya nae mapenzi.
Ameeleza kuwa moja kati ya ishara hizo ni pale walipokuwa wakishikana
mikono kusalimiana, alikuwa anambinya au kumtekenya katikati ya
kiganja.
Katika nyaraka hizo ameendelea kueleza kuwa MJ alikuwa anamchukua na
kumpeleka kwenye majumba ikiwa ni pamoja na sehemu inayoitwa ‘The
Hideout’ ambapo walikuwa wakinywa vinywaji laini, pink wine na kuangalia
video za ngono.
Amesema marehemu aliendelea kumfanyia vitendo hivyo hadi pale alipoanza kubalehe.
Hata hivyo, mwanasheria wa Michael Jackson, Howard Weitzman ameiambia
TMZ kuwa kesi hiyo inatakiwa kutupiliwa mbali kwa kuwa imeletwa kwa
mara ya kwanza miaka 20 baada ya tukio hilo analolieza na kwamba James
Safechuck aliwahi kula kiapo na kueleza kuwa Michael Jackson hakumfanyia
kitu chochote kibaya.
0 comments:
Chapisha Maoni