Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba
linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia
Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad
alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12
na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani
(Dola moja ni wastani wa Sh1,650).
Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400
sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12
vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana,
gharama hizo zitafikia Sh142.56.
Vifaa vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa, vilikuwa siyo standard (viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka Ukumbi wa Mikutano wa AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifungaalisema.
Alisema tangu wavifunge, hawajawahi kupata
malalamiko tena kutoka katika kamati kuhusu ubora na kwamba gharama za
kukodisha vifaa hivyo itatoka katika fungu la dharura la Bunge Maalumu.
Mara ya kwanza walituambia gharama zao ni Dola 500 kwa siku lakini tukajadiliana nao, hivyo tukafikia kiwango hicho cha Dola 450alisema.
Hamad alisema vifaa vya awali ambavyo
vililalamikiwa na wajumbe kuwa havitoshi, vinatoa sauti nje ya majengo
na kwa jinsi vilivyo, vinalazimika kutembezwa ukumbini, hivyo
kusababisha usumbufu.
Malalamiko ya gharama
Suala la gharama limekuwa likiibuka mara kwa mara
na wakati mwingine kutajwa kama sababu ya kuahirishwa kwa Bunge hilo kwa
kuwa hakuna uhakika wa kupatikana kwa akidi inayotakiwa kufikia uamuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba
alilalamikia kile alichokiita “matumizi ya kufuru” ya Bunge Maalumu
wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa Katiba Mpya.
Kibamba alisema ikiwa Bunge litaendelea na vikao
vyake hadi Oktoba 31, mwaka huu kama ratiba inavyoonyesha, sehemu hiyo
ya mchakato itakuwa imeligharimu taifa Sh40 bilioni, fedha ambazo
zingetosha kugharimia maji kwa wananchi wote wa Wilaya za Kondoa mkoani
Dodoma na Kilindi, Tanga.
Tatizo kubwa hapa ni posho, kila mara sheria na kanuni zimekuwa zikibadilishwa ili kuongeza muda wa Bunge siyo kwa ajili ya kitu kingine, bali kwa ajili ya posho, kwa hiyo gharama zinazidi kuongezeka na haya ni matumizi ya kufuru ambayo hayapaswi kufanywa katika nchi maskini kama yetualisema Kibamba na kuongeza:
Katika awamu ya kwanza, zaidi ya Sh10 bilioni zilitumika na sasa fedha zilizotengwa kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Fedha (Mwigulu Nchemba) ni Sh20 bilioni na hizo zilitengwa kwa siku 60 tu lakini kwa siku zilizoongezwa hadi kufikia kati ya 84 na 90, gharama zitaongezeka kwa zaidi ya Sh10 bilioni.
Bunge kuajiri 10
Katika hatua nyingine, Bunge Maalumu linakusudia
kuajiri wataalamu 10 kutoka nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na
Baraza la Wawakilishi ili kusaidia utekelezaji wa majukumu yake.
Hamad alisema ulazima huo unatokana haja ya kupata watu wa kusaidia kwenye kamati na kwenye uandishi.
0 comments:
Chapisha Maoni