KAMA hakuwahi kutoa sadaka, huu ndiyo muda wake! Staa
wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani
kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu,
Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul
‘Diamond’.
Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo
lilijiri Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo
Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo
aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana,
Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo
timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla
waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao
walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa
peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza
Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini
walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man
ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali
na waume za watu.
Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini,
Wema alitoka na msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo
waliwaambia wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa
kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na
kuanza kuchati naye hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada ya kujazwa data hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwengi
ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda
kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama
angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa
na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto
akamfanyie shopping.
Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni
kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni
Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine
kimejificha.
Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.
Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu
alisema Mwengi.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi:
Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.
0 comments:
Chapisha Maoni