Kwa siku ya mpili mfululizo kumekua na mapambano
katika mji wa Missouri nchini Marekani kufuatia kifo cha kijana mmoja
mweusi ambaye alipigwa risasi na polisi katika kitongoji cha St Louis
siku ya jumamosi.
Mkuu wa polisi wa kitongoji cha watu weusi cha
Ferguson,Tom Jackson amesema kwamba polisi walitumia gesi na risasi za
bandia ili kuwatawanya watu waliokua wamefurika karibu na jengo ambalo
liliteketezwa kwa moto siku ya tukio ambapo maduka yaliporwa bidhaa na
magari yaliharibiwa vibaya.
Ni wakati huo wa utumizi wa gesi na risasi
bandia ndipo raia walipoamua kuwarushia mawe polisi,polisi nao wakajibu
mapigo kwa kuwarushia risasi raia hao.
Kijana Michael Brown,alipigwa risasi kadhaa
alipokua amening'inia kwenye gari ya polisi,na kufuatia tukio hilo FBI
wanachunguza endapo kuna uvunjifu wa haki za binadamu katika tukio hilo
la kuuawa kwa kijana Michael Brown.
0 comments:
Chapisha Maoni