UWEPO wa chombo maalum, umetajwa kama njia pekee ya kutatua kero za
wanawake ambao kwa muda mrefu wamekandamizwa na mfumo dume, hivyo
kubaki nyuma kiuchumi na kiuongozi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa
na Utawala, Dk. Alexander Makulilo ndiye alitoa rai hiyo wakati
akizungumza kwenye mjadala kuhusu mchakato wa katiba mpya.
Mjadala huo uliandaliwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na
Watoto (WLAC) kwa msaada wa Shirika la kimataifa la OXFAM na
kuwakutanisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa muda mrefu kumekuwa na fikra potofu, kwamba wanawake
hawana uwezo ingawa kuna ushahidi wa wale ambao wamepewa nafasi na
wamefanya vizuri.
Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, baadhi ya tafiti zilizofanywa mwaka
2013 na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya
Demokrasia (TCD), zimeonyesha kuwa wanawake wanachagulika iwapo
watagombea nafasi mbalimbali za uongozi.




0 comments:
Chapisha Maoni