MKUU wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Venance Mwamoto, amevamia
jukwaa la mkutano wa NCCR-Mageuzi na kisha kumtolea lugha ya matusi
Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali.
Mwamoto alijikaribisha kwenye mkutano huo uliokuwa ukihutubiwa na
Katibu Mkuu, Mosena Nyambambe kisha akaketi kiti cha mbele walipokuwa
viongozi wengine wa chama hicho na kuanza kumchokoza Mkosamali kwa
kumtolea lugha chafu kwa sauti ya chini.
Mkuu huyo wa wilaya anadaiwa kufikia hatua hiyo ya kuporomosha matusi
kwa kilichoelezwa kuwa alituhumiwa na Mkosamali kwenye mkutano, kwamba
amejimilikisha isivyo halali ekari 73 za ardhi katika Kijiji cha Nduta
wakati tayari anatumia wanajeshi kuwaondoa wanakijiji hao kwa kile
kilichodaiwa ni kutaka kubadili matumizi ya ardhi ili kijiji hicho kiwe
hifadhi.
Sokomoko hilo lilimalizwa kwa busara za wabunge, David Kafulila
(Kigoma Kusini) na Moses Machali (Kasulu Mjini) baada ya Mwamoto na
Mkosamali kukaribia kuzichapa kavu kavu jukwaani.




0 comments:
Chapisha Maoni